Jopo la ushauri la Marekani linasema Korea Kaskazini ilifanya jaribio la injini ya roketi mwezi Aprili

Jopo la ushauri wa kitaalam la Marekani linasema Korea Kaskazini imefanya jaribio la kuwasha injini ya roketi mwishoni mwa mwezi Aprili katika kituo cha kurushia satelaiti cha Sohae kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Kituo cha Masomo ya Kimkakati na Kimataifa, au CSIS, kilitoa matokeo hayo juzi Jumatatu kutoka katika uchanganuzi wa picha za satelaiti za kituo hicho. Picha hizo zilipigwa Aprili 29.

Watafiti wa CSIS wanasema walithibitisha mimea iliyoungua na makovu ya ardhini karibu na kifaa cha kufanya majaribio ya injini. Wanasema pia picha hizo na vyanzo kadhaa vinaashiria kuwa lilifanyika jaribio la injini ya roketi inayoendeshwa kwa kutumia fueli ya kimiminika.

Jeshi la Korea Kusini liliwaambia waandishi wa habari jana Jumanne kwamba lilikuwa linafahamu kuhusu jaribio la kuwasha injini katika kituo hicho cha.

Jeshi hilo lilisema Korea Kaskazini inafanya maandalizi ya kurusha
satelaiti nyingine ya kijeshi ya kijasusi, ingawa hakuna dalili za kurushwa hivi karibuni.
###