Mkuu wa UN atoa wito kwa Israel na Hamas kutopoteza fursa ya makubaliano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN Antonio Guterres ametoa wito wa dhati kwa Israel na Hamas kutopoteza fursa ya makubaliano ya kusitisha vita na kuachiliwa kwa mateka.

Akiwahutubia waandishi wa habari jana Jumatatu, Guterres alisema kuwa mapema siku hiyo alitoa “wito wa dhati zaidi kwa serikali ya Israel na uongozi wa Hamas ili kupiga hatua kubwa katika kufanikisha makubaliano ambayo ni muhimu kabisa.”

Ameielezea fursa hiyo kuwa “fursa ambayo haiwezi ikapotezwa.”

Guterres ameongeza kwamba uvamizi wa ardhini katika mji wa Rafah uliopo kusini mwa eneo la Gaza “hautavumiliwa kwa sababu ya madhara yake mabaya kwa binadamu na kwa sababu ya athari yake ya kusababisha ukosefu wa uthabiti katika eneo hilo.”
###