Inoue Naoya amshinda Luis Nery na kutetea taji la pamoja la uzani wa super bantam

Bondia Mjapani Inoue Naoya ametetea taji lake la pamoja la ubingwa wa uzani wa super bantam kwa mara ya kwanza kwa kumshinda Luis Nery wa Mexico kwa technical knockout katika raundi ya sita ya mpambano huo uliofanyika jijini Tokyo jana Jumatatu.

Inoue alishinda mataji yote maarufu manne ya kitengo cha uzani wa super bantam mwaka jana, baada ya kuwa bingwa wa taji la pamoja katika uzani tofauti. Nery ni bingwa wa zamani wa dunia katika vipengele viwili vya uzani.

Nery alimwangusha Inoue kwenye raundi ya kwanza kwa ngumi ya kushoto. Lakini Inoue aliamka na kumwangusha Nery katika raundi iliyofuata kwa ngumi ya kushoto. Ngumi nyingine ya kushoto kutoka kwa Inoue ilimfanya mpinzani wake wa Mexico arambe sakafu tena katika raundi ya tano.

Katika raundi ya sita, Inoue alimpeleka Nery kwenye kona na kummaliza kabisa kwa ngumi ya mkono wa kulia.
###