Uchaguzi wa urais Marekani: Imebaki miezi 6, Trump aongoza kidogo kwenye kura za maoni

Ikiwa imebaki miezi sita kabla ya kinyang’anyiro cha urais nchini Marekani, kura za maoni zinaonyesha Rais wa zamani Donald Trump ameongoza kwa kura kidogo dhidi ya Rais Joe Biden.

Trump anayedhaniwa kuja kuwa mgombea wa urais wa Republican amekuwa akihudhuria kesi zake za uhalifu, huku akiendesha kampeni yake.

Hivi karibuni amekuwa akitembelewa na viongozi wa kigeni.

Rais wa Poland Andrzej Duda na Makamu wa Rais wa Chama Kikuu Tawala cha Japani cha Liberal Democratic, Aso Taro, ni miongoni mwa viongozi waliomtembelea Trump hivi karibuni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron pia alimtembelea.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii kuhusu mazungumzo yake na Trump.

Mjapani mmoja mtaalam wa masuala ya siasa za Marekani amesema ziara za viongozi hao wa nje ya Marekani zinasaidia kampeni ya Trump.