Bendera kubwa zenye umbo la samaki zawavutia wengi mkoani Saitama

Bendera zenye umbo la samaki za rangi nzuri hupeperushwa kote nchini Japani wakati huu wa mwaka kwa ajili ya Siku ya Watoto, yaani siku ya Mei Tano. Lakini ikiwa ungependa kuona mojawapo kubwa zaidi, nenda Jiji la Kazo katika Mkoa wa Saitama.

Wenyeji walirusha bendera hiyo kubwa angani jana Ijumaa kwa kutumia winchi. Bendera hiyo ina urefu wa mita 100 na uzito wa kilo 330.

Asubuhi, upepo ulikuwa dhaifu sana. Lakini mchana, bendera hiyo ilianza kuelea, ikifurahisha wale walioitazama.

Jiji la Kazo linasifika kwa kutengeneza bendera hizo.