Kishida na Lula wakubaliana kushirikiana katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Waziri Mkuu wa Japani Kishida Fumio amekutana na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva kwa mazungumzo yaliyolenga zaidi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Viongozi hao wawili walikutana jijini Brasilia nchini Brazil jana Ijumaa. Kishida alisisitiza juu ya umuhimu wa ushirikiano na Brazil.

Nje ya Japani, Brazil ina jumuiya kubwa ya watu wenye asili ya Japani.

Kishida alisema, “Nitatumia mazungumzo ya mkutano huu na Rais Lula kama fursa ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande mbili. Nimefufua upya ahadi yangu.”

Brazil inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wa Umoja wa Mataifa, COP30 utakaofanyika mwakani.

Kishida na Lula walikubaliana kupanga kusaidia kujifadhi mto wa Amazon, ikiwemo hatua za kuzuia ukataji wa miti na kurejesha ardhi iliyoharibika.

Pia walikubaliana juu ya mpangokazi wa pande mbili unaolenga katika kusaidia dunia kuondokana na hewa ya kaboni. Japani itaangazia kunufaika na nishati ya mimea na maliasili nyingi za Brazil. Na Brazil itaangazia teknolojia ya hali ya juu ya Japani, ikiwemo injini za mseto.

Mengineyo katika mazungumzo hayo, Kishida na Lula waliahidi kudumisha utaratibu huru na wazi wa dunia kwa kuzingatia utawala wa sheria.