Mawaziri wa OECD watoa hadhari ya kulazimishwa kiuchumi

Mawaziri wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo OECD wamehitimisha mkutano wao wa siku mbili jijini Paris nchini Ufaransa kwa taarifa inayoelezea “wasiwasi mkubwa” juu ya kulazimishwa kiuchumi.

Japani ilikuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la kundi la wanachama 38 mwaka huu. Mazungumzo hayo yalihitimishwa jana Ijumaa.

Mawaziri hao walishutumu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine “kwa maneno yenye nguvu kwa kadiri iwezekanavyo.”

Pia walielezea “wasiwasi wao mkubwa” juu ya athari hasi kwa migogoro ya Mashariki ya Kati.
Mawaziri hao walithibitisha kujitolea kwao kujenga uthabiti wa kiuchumi na usalama.

Ulazimishaji wa kiuchumi unarejelea hatua za kushinikiza wadau wa biashara kupitia vizuizi ama ushuru.

Huku ikionekana kuizingatia China, mawaziri hao waliahidi kuhakikisha kwamba majaribio ya kutegemea silaha za kiuchumi yatashindwa.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Kamikawa Yoko alisema Japani ilichangia kufanya mazungumzo yawe yenye tija licha ya kuongezeka kwa tofauti kwenye jumuiya ya kimataifa.

Aliongeza kwamba mkutano huo umeweka msingi wa kubadilishana mawazo katika nyanja ya usalama wa uchumi.