Japani na EU zakubaliana kulinda mitungo ya usambazaji

Mawaziri wa Japani Kamikawa Yoko wa Mambo ya Nje na Saito Ken wa Uchumi, Biashara na Viwanda jana Alhamisi mjini Paris nchini Ufaransa walikutana na Makamu wa Rais Mtendaji wa Tume ya Ulaya Valdis Dombrovskis.

Walielezea mashaka juu ya kutegemea nchi kama vile China kwa vile wanavyoviita “bidhaa za kimkakati,” ikiwa ni pamoja na semikondakta na madini muhimu.

Pia wameshuhudia baadhi ya kampuni zikiyafanya masoko kufurika na bidhaa za bei rahisi, kwa hivyo wanataka kutoangazia mno bei. Wanapanga kufanya kazi kuelekea mazingatio mengine kama vile kuhifadhi mazingira na ulinzi dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni.

Mwezi Aprili mwaka huu, viongozi wa Japani na Marekani walithibitisha tena dhamira yao ya kuimarisha mitungo ya usambazaji wa madini muhimu. Wanapanga kufanya kazi na wenzao katika Umoja wa Ulaya, EU juu ya seti ya kanuni za pamoja kwa ajili ya usalama wao wa kiuchumi.