Kishida na Macron wakubaliana kuanza mazungumzo juu ya mpango wa ushirikiano wa kiusalama

Waziri Mkuu wa Japani Kishida Fumio jana Alhamisi alikutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa chakula cha mchana katika Ikulu ya Rais mjini Paris.

Viongozi hao walijadiliana juu ya kufanya mazungumzo ya pande mbili ili kujiandaa kwa Makubaliano ya Ubadilishanaji yanayoweza kufikiwa.

Mkutano wao unakuja wakati kukiwa na ongezeko la shughuli za China baharini katika Asia-Pasifiki. Wachambuzi wa mambo wanasema Ufaransa inatafuta kuimarisha tena ushirikiano wa kiusalama na Japani katika eneo hilo kwa kuzingatia maeneo yake ya nje ya nchi katika Pasifiki Kusini ikiwa ni pamoja na New Caledonia.

Kishida na Macron pia walikubaliana kudumisha ushirikiano wa karibu kwa masuala mengine kama vile Korea Kaskazini na pia hali katika Mashariki ya Kati na nchini Ukraine.

Viongozi hao walielezea tumaini kuwa mabadilishano kati ya vijana na wengineo yataongezeka kupitia michezo ya mwaka huu ya Olimpiki na Paralimpiki mjini Paris, Maonyesho ya Dunia yatakayofanyika mwakani mjini Osaka nchini Japani na matukio mengine.