Benki Kuu ya Marekani haijabadilisha viwango vya riba

Maafisa wa Benki Kuu nchini Marekani wametumia nyenzo zao kujaribu kupunguza bei ya juu. Walifanikiwa kwa wakati fulani, lakini hatua yao katika mfumuko wa bei ilikwama. Sasa, wameamua kutobadili viwango hivyo vya riba.

Watunga sera katika benki hiyo kuu wamepandisha viwango vya riba hadi kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha zaidi ya miaka 20. Hata hivyo, jana Jumatano, kwa mkutano wa sita mfululizo, waliamua kuviacha bila kubadili.

Watunga sera walitoa taarifa wakisema wamekabiliwa na "ukosefu wa upigaji hatua zaidi" juu ya kupanda kwa bei na kwamba wanahitaji kuwa na uhakika zaidi kuwa mfumuko wa bei unakwenda "kiuendelevu" kuelekea lengo lao la asilimia 2.