Ruto awatembelea waathirika baada ya watu 48 kufariki katika mafuriko makubwa magharibi mwa Kenya

Huko Mai Mahiu, magharibi mwa Kenya, mafuriko makubwa ya Aprili 29 yamesababisha vifo vya watu 48 hadi kufikia sasa.

Rais William Ruto wa Kenya jana Jumanne Aprili 30, aliwatembelea waathirika na kutoa wito wa kuhama kutokana na utabiri wa hali ya hewa kuonyesha mvua zaidi kunyesha.

Kwa mujibu wa Ruto, idadi ya vifo imefikia 171 nchini Kenya kutokana na mvua kubwa na mafuriko yanayoendelea tangu mwezi Machi.