Maswali na Majibu: Magonjwa ya kupe (5)

(5) Hatua za uzuiaji: dawa za kuzuia wadudu

NHK inajibu maswali yanayohusiana na kuhakikisha usalama katika maisha yetu ya kila siku. Magonjwa yanayoenezwa na kupe wanaoishi katika maeneo ya misitu na mashamba yamekuwa yakiongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Magonjwa haya yanaweza yakasababisha dalili kama vile homa ama kuharisha na huenda yakasababisha kifo katika baadhi ya visa. Mfululizo huu unajadili masuala ya kuzingatia na njia ya kuzuia kuumwa na kupe. Katika kipengele hiki cha mwisho, tunaangazia dawa za kuzuia wadudu.

Dawa za kuzuia wadudu zinazonyunyizwa ni fanisi katika kuwazuia kupe. Miongoni mwa vitu maarufu vilivyo kwenye dawa hizo ni “DEET” na “Icaridin.” Dawa za kunyunyiza zilizo na vitu hivi zinapatikana katika maduka ya kuuza dawa, na kadhalika. Tafadhali, changua bidhaa ambayo inakidhi mahitaji yako. Unapotumia DEET, hakikisha unaangalia vizuizi vya umri na ukomo wa matumizi kwa siku. Mbali na kuitumia moja kwa moja kwenye ngozi yako, dawa za kuzuia wadudu pia ni fanisi wakati zinaponyunyizwa kwenye mavazi au viatu vyako. Hata hivyo, ni vigumu kuzuia kuumwa na kupe kwa kutumia tu dawa za kuzuia wadudu. Tafadhali pia chukua hatua zingine kama vile kuvaa mavazi yanayostahili.
Taarifa hii ni sahihi hadi kufikia Aprili 30, 2024.