Maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kufanyika katika miji kulikodondoshwa mabomu ya atomiki

Imetimia miaka 30 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Katika mwaka huu wa kumbukumbu, matukio ya maadhimisho kwa mara ya kwanza yatafanyika katika miji ya Hiroshima na Nagasaki kulikododondoshwa mabomu ya atomiki.

Miaka 30 tangu kutokea kwa mauaji hayo, Ubalozi wa Rwanda nchini Japani na pande zingine zinapanga kufanya matukio hayo ili kutoa tumaini lao la amani katika eneo ambalo binadamu ameshuhudia majanga.

Matukio hayo yatafanyika katika Chuo Kikuu cha Hiroshima City mjini Hiroshima Mei 25 mwaka huu na katika Makumbusho ya Bomu la Atomiki ya Nagasaki mjini Nagasaki Juni 17.

Maandalizi yanafanyika ili manusura wa mabomu hayo ya atomiki na Balozi wa Rwanda waweze kushiriki matukio hayo.

Towari Marie-Louise, mwenyekiti wa mmoja wa mwandalizi mwenza “Think About Education RWANDA”, shirika lisilokuwa la kujipatia faida, amesema anatumai kuwa watu wengi watashiriki ili machungu ya vita vilivyoshuhudiwa na watu wa Rwanda, Hiroshima na Nagasaki yawasilishwe kwao. Hiyo itasaidia ulimwengu kamwe kutorudia makosa hayo tena.