Safari za boti za Shiretoko zaanza tena huku kukiwa na hatua mpya za usalama

Waendeshaji wa boti za utalii katika mji wa Shari mashariki mwa Hokkaido wamerejesha shughuli kwa msimu huu.

Takribani abiria 60 walipanda kwenye boti mbili jana Jumapili. Walikuwa na kifaa cha mkononi kinachotoa taarifa ya eneo lao kwa meli zingine ikiwa kutakuwa na tukio la dharura.

Chama cha waendeshaji boti za watalii katika bandari ya Utoro huko Shari kinafuata sheria kadhaa za usalama kilichojiwekea baada ya boti ya watalii kuzama na kusababisha vifo kwenye Rasi ya Shiretoko mwaka 2022. Chama hicho kinatumia kifaa hicho kuanzia msimu huu.

Abiria wanaweza kutuma taarifa za eneo lao kwa kampuni zingine za boti za watalii au boti za uvuvi, kwa kutumia mfumo wa GPS ikiwa watabonyeza kitufe kwenye kifaa hicho.