Yeni yashuka hadi kiwango cha 160 dhidi ya dola

Sarafu ya yeni ya Japani imezidi kudhoofika dhidi ya dola ya Marekani katika soko la kubadilisha fedha za kigeni leo Jumatatu, ikishuka hadi kiwango cha 160 wakati fulani.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 34 kwa sarafu hiyo kufika kiwango cha yeni 160 dhidi ya dola.