Jopo la Ushauri la Marekani: Urusi huenda isiweze kuielemea Ukraine kabla ya msaada wa Marekani kuwasili

Vikosi vya Urusi vinashambulia majiji katika eneo la Kharkiv mashariki mwa Ukraine pamoja na maeneo muhimu ya mstari wa mbele wa mapigano. Maafisa wa intelijensia wa Ukraine wameripotiwa wanasema kwamba Urusi huenda “ikajiandaa kwenye uwanja wa vita” kabla ya mashambulizi makubwa mwishoni mwa Mei au Juni.

Jopo la ushauri la Marekani, ambalo ni Taasisi ya Utafiti wa Vita, juzi Jumamosi lilisema “vikosi vya Urusi huenda vikapata faida muhimu ya kimkakati katika majuma yajayo wakati Ukraine ikisubiri msaada wa kiusalama kutoka Marekani kuwasili katika mstari wa mbele wa mapigano” lakini huenda isielemee ulinzi wa Ukraine kutokana na zana za zamani na wanajeshi wenye mafunzo duni.

Pia linasema “Ukraine ina uwekezekano mkubwa wa kuimarisha mistari ya mbele ya mapigano katika miezi ijayo na huenda ikaweza kuanza operesheni ndogo ya mashambulizi ya kujibu mwishoni mwa 2024 au mwanzoni mwa 2025.”

Hivi karibuni utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden ulitangaza msaada wa nyongeza wa kijeshi kwa Ukraine.