Maji yaliyochanganyika na dutu kali kutoka mtambo wa Fukushima Namba Moja yapungua hadi kufikia 1/6

Mwendeshaji wa mtambo wa nishati ya nyuklia wa Fukushima Namba Moja ulioharibika amesema amefanikiwa moja ya malengo yake ya kudhibiti mtiririko wa maji yaliyochanganyika na dutu kali za mionzi.

Mwendeshaji huyo amesema uwingi wa maji ya kila siku hivi sasa ni chini ya moja ya sita ya kipindi maji yanaingia kwa wingi zaidi

Maji hayo yaliyochanganyika yamekuwa yakikusanywa katika mtambo huo tangu uliokumbwa na uyeyukaji mara tatu kufuatia tetemeko kubwa la ardhi na tsunami la mwaka 2011.

Maji hayo yalikuwa yakitumika kupoozea kimiminika cha fueli ya nyuklia kilichochanganyika na maji ya mvua na maji ya ardhini ambayo hutiririka kuingia katika majengo ya kinu kilichoharibika, na kutengeneza maji yaliyochanganyika na dutu hizo.

Kampuni ya Umeme ya Tokyo TEPCO ambaye ndiye mwendeshaji wa mtambo huo amesema kiwango cha wastani cha kila siku cha maji yanayokusanywa kilikuwa takribani tani 80 katika mwaka wa fedha wa 2023 ambacho kiliishia mwezi Machi mwaka huu.

Kiwango kikubwa cha kila siku kilikuwa ni tani 490 kilichorekodiwa katika mwaka wa fedha wa 2015.

Kampuni hiyo imesema upunguaji unatokana na udhibiti mzuri wa uwingi wa maji ya mvua na ardhini kwa kufunika uso wa ardhi kwa zege maeneo ya majengo.

TEPCO imekiri kiwango cha mvua za mwaka kwa mwaka jana kilikuwa chini ya wastani, lakini inakadiria kuwa ukusanywaji wa maji hayo kila siku hautazidi tani 90, hata kama kituo kina kiwango kikubwa cha mvua.

Serikali na TEPCO zimesema zimefanikisha moja ya malengo yaliyowekwa katika muda wa kuufunga mtambo huo, ambao ni kuendeleza kiwango cha kila siku cha maji yaliyochanganyika na dutu kali kuwa chini ya tani 100 ifikapo mwaka 2025.

Hata hivyo, hakuna matumaini yanayoonekana ya kusitisha kabisa maji hayo.

TEPCO imesema inapanga kuweka tandiko kubwa juu ya majengo ikiwa ni juhudi za kupunguza zaidi kiwango cha kila siku cha maji hadi kufikia tani 70 ama chini ya hapo ifikapo Aprili 2029.