Udhaifu wa yeni waleta chaguzi kwenye msimu wa sikukuu nchini Japani

Sikukuu za msimu wa chipukizi zimeanza nchini Japani. Mapumziko hayo yanakuja wakati sarafu ya yeni ikidhoofika hadi kufikia wastani wa 158 dhidi ya dola jijini New York, na kufanya kuwa chini zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 34. Sarafu hiyo ya Japani inaleta neema kwa watalii wengi wa kigeni ambao wamekuwa wakimiminika katika maeneo ya kitalii.

Mji wa kihistoria wa Kawagoe upo takribani saa moja kutoka katikati mwa Tokyo. Nyumba za wakazi wa mji huo zilizo na mtindo wa kizamani ni kivutio kikubwa.

Kushuka thamani kwa yeni sasa kunawapa watalii wanaoingia katika mji huo sababu zaidi za kufurahia muda wao nchini Japani.

Mtalii mmoja kutoka nje ya nchi aliiambia NHK kuwa udhaifu wa yeni unafanya iwe rahisi kwao kufanya manunuzi na kutembelea maeneo mengi nchini Japani.

Ikiwa wasafiri wa kigeni watafurahia, inakuwa ngumu kwa wageni wa Kijapani kufurahia pamoja hali hiyo.

Mwanamke mmoja aliyeolewa hivi karibuni alisema, “Ninataka kweli kusafiri kwenda nje ya nchi lakini si rahisi hivyo sasa.”

Wanandoa wa Kijapani wanahisi maumivu ya kiwango cha kubadili fedha katika wiki moja yao ya kukaa Hawaii.

“Wakati mwingine hatukupata kifungua kinywa na tuliunganisha chakula asubuhi na mchana, ili kuokoa fedha za kula,” alisema mwanamke huyo. “Na wakati mwingine kifungua kinywa chetu ni chakula cha kupasha tulichokuja nacho kutoka Japani. Ikiwa kiwango cha kubadili fedha kingekuwa kidogo bora, safari yetu ingekuwa rahisi zaidi.”

Utafiti uliofanywa na wakala mkubwa wa usafiri JTB unasema zaidi ya asilimia 70 ya waliojibu utafiti huo wanachagua kutosafiri usiku. Utafiti huo unasema watu wengi wanagusia changamoto za kiuchumi kulinganisha na mwaka jana.