Yeni yashuka hadi wastani wa 158 dhidi ya dola, mwaka wa 34 mfululizo ikiwa chini

Sarafu ya Japani imeshuka hadi 158 dhidi ya dola kwenye soko la New York jana Ijumaa, kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu mwezi Mei mwaka 1990, baada ya Benki ya Japani, BOJ kuamua kutobadilisha sera ya kifedha.

Uamuzi wa BOJ na maoni ya Gavana wa BOJ Ueda Kazuo aliyoyatoa baadaye kwenye mkutano na wanahabari yalipekea fununu kwamba BOJ haitaongeza viwango vya riba katika siku za karibuni.

Wafuatiliaji wa soko wanaamini pengo la kiwango cha riba kati ya Marekani na Japani linawezekana likasalia kwa sasa, na kusababisha hatua za kununua dola yenye faida kubwa.