Jitihada za kujitolea katika eneo la Noto lililoathiriwa na tetemeko kuongezwa kasi wakati wa likizo ya majira ya chipukizi

Likizo ndefu ya majira ya chipukizi inayojulikana kama Wiki ya Dhahabu nchini Japani imeanza leo Jumamosi, na baadhi ya watu watatumia likizo zao kujitolea katika maeneo ya Mkoa wa Ishikawa yaliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi.

Maafisa wanasema zaidi ya watu 70,000 wamejitolea katika maeneo yaliyoathiriwa tangu maafa hayo kutokea Siku ya Mwaka Mpya.

Wamesaidia kuondoa taka, kusafirisha bidhaa na kusaidia vituo vya uokoaji.

Baadhi ya wakaazi wa Jiji lililoathiriwa sana la Wajima wataanza kuhamia katika nyumba za muda kuanzia leo Jumamosi.

Maafisa wa eneo hilo wameweka vipeperushi kwenye kumbi za jiji na vituo vingine vinavyotumika kama vituo vya kujihifadhi, wakiwaambia waombe usaidizi kwa watu wa kujitolea.

Chuo kikuu kimoja jijini Tokyo kinapanga kutuma wanafunzi 16 katika Mji wa Noto.

Mwanafunzi mmoja anasema ataweza kusaidia kusogeza vitu vizito. Mwingine anasema amekuwa akitaka kuzuru eneo hilo na kusaidia.