Biden aiahidi Ukraine msaada wa kijeshi ‘mara moja’

Rais wa Marekani Joe Biden jana Jumatano amesaini kuwa sheria msaada wa kigeni unaojumuisha msaada kwa Ukraine wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 60. Hatua hiyo inakuja baada ya miezi kadhaa ya wabunge kubishana.

Biden aliidhinisha usafirishaji wa awali wa magari ya kivita na silaha kwa ulinzi wa anga, mizinga mikubwa na mifumo ya roketi yenye thamani ya dola bilioni moja. Alisema atahakikisha kwamba upelekaji unaanza “mara moja.”

Viongozi wa Ukraine wanasema watafanya kila wawezalo kufidia muda uliopotea.

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine alisema, “Ninamshukuru Rais Biden na Bunge, kwa Wamarekani wote walioona umuhimu wa kumshinda Putin.”

Viongozi wa Urusi wamesema upelekaji huo wa silaha hautabadili hali kwenye mistari ya mbele vitani. Tayari wamekwisha ahidi kulenga kambi zinazohifadhi silaha za Marekani.