Maswali na Majibu: Maambukizi ya kupe (2)

(2) Nini cha kufanya unapong’atwa na kupe

NHK inajibu maswali kuhusiana na kuhakikisha usalama katika maisha ya kila siku. Magonjwa yanayoambukizwa na kupe wanaoishi katika maeneo ya msitu na mashamba yamekuwa yakiongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Wakati unapoambukizwa, dalili huenda zikajumuisha homa au kuharisha ambazo zinaweza zikasababisha kifo hali ikiwa mbaya zaidi. Mfululizo huu unajadili tahadhari unazopaswa kuchukua na hatua za uzuiaji. Katika sehemu ya pili tutaangalia nini cha kufanya unapong’atwa na kupe.

Kupe hujishikiza wenyewe kwenye mwili wa mtu ama mnyama mwingine, na hunyonya damu kwa saa nyingi. Inasemekana mtu anayeng’atwa mara nyingi hafahamu kuwa ameng’atwa.

Mara tu unapogundua umeng’atwa na kupe, unapaswa kwenda kwa daktari wa ngozi ama hospitali mara moja ili kupe huyo aondolewe inavyostahili, kidonda kitibiwe na upate tiba nyingine yoyote muhimu. Usijaribu kumwondoa kupe kwa kuwa sehemu za kupe huyo zinaweza kusalia ndani ya ngozi yako na kidonda kitatunga usaha.

Baada ya kutibiwa, unapaswa kuendelea kuangalia mabadiliko yoyote ya mwili wako kwa kipindi cha wiki chache. Nenda hospitali wakaangalie ikiwa utapata dalili zozote ikiwa ni pamoja na homa.

Taarifa hii ni sahihi hadi kufikia Aprili 24, 2024.