Tetetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 latokea mashariki mwa Taiwan leo Jumanne

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 kwenye kipimo cha Richter limetokea mashariki mwa Taiwan mapema leo Jumanne asubuhi.

Mamlaka Kuu ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Taiwan imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na kaunti ya mashariki ya Hualien muda mfupi baada ya 8:30 usiku kwa saa za eneo hilo.

Tetemeko hilo lilisajili ukubwa wa alama karibu na 5 huko Hualien na 3 huko Taipei kwenye kipimo cha matetemeko cha Taiwan kinachoanzia sifuri hadi saba.

Hadi kufikia sasa, hakujakuwa na ripoti za uharibifu.