Wizara ya Ulinzi ya Japani yasema vyombo vya kurekodia safari ya helkopta zilizoanguka vyapatikana

Wizara ya Ulinzi ya Japani imesema kwamba vyombo viwili vya kurekodia safari ya helkopta vimepatikana, sambamba na mabaki mengine ambayo yanaaminika kutoka katika helkopta mbili za Kikosi cha Kujihami Majini ambazo zilianguka.

Mawasiliano na helkopta hizo yalipotea jana Jumamosi usiku pale zilipokuwa takribani kilomita 270 mashariki mwa Kisiwa cha Torishima katika Bahari ya Pasific.

Wizara hiyo imesema vitunza sauti hivyo vilipatikana katika maeneo ya karibu na inapoweza kutokea ajali ya angani.

Helkopta hizo aina ya SH-60K kila mmoja ikiwa na watu wanne zilikuwa katika mafunzo ya usiku ya kutafuta nyambizi.

Mtu mmoja aliokolewa lakini baadaye alifariki.

Wizara hiyo inaendelea kuwatafuta watu wengine saba na itatathmini taarifa kutoka katika vitunza sauti hivyo.

Kikosi cha Kujihami cha Majini kimezizuia helkopta zote za aina ya SH-60K.