Vyombo vya habari vya Iran: Milipuko imesikika katika jimbo la kati

Chombo cha habari cha Fars cha Iran leo Ijumaa kimeripoti kuwa milipuko imesikika katika mji wa Isfahan.

Mji huo unapatikana takriban kilomita 350 kusini ya Tehran.

Milipuko hiyo iliripotiwa kusikika karibu na uwanja wake wa kimataifa wa ndege. Mji wa Isfahan pia kuna kambi kubwa ya jeshi la anga la Iran.

Vyombo vingine vya habari vya Iran vinasema safari za ndege zimesitishwa katika miji kadhaa.

Hii inakuja baada ya Israel kuapa kulipiza kisasi kufuatia shambulizi la droni na kombora lililotekelezwa na Iran mwishoni mwa wiki iliyopita. Lakini haijabainika kilichosababisha milipuko hiyo au ikiwa Israel imehusika.