Polisi jijini Tokyo yatuma nyaraka mahakamani za mshauri wa zamani wa ubalozi wa Singapore

Polisi jijini Tokyo imetuma nyaraka kwa waendesha mashtaka kuhusu mshauri wa zamani wa Ubalozi wa Singapore nchini Japani anayetuhumiwa kuchukua video kwa siri ya kijana aliye uchi kwenye bafu la umma jijini humo.

Idara ya Polisi Jijini Tokyo ilimtaja Sim Siong Chye kwa waendesha mashtaka leo Alhamisi kwa kushukiwa kukiuka sheria zinazopiga marufuku biashara ya ngono ya watoto na masuala mengine.

Polisi wanasema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 55 anatuhumiwa kuchukua video ya mvulana huyo na wengine kwa simu yake ya smartphone kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha bafu la umma mnamo mwezi Februari. Alikuwa akifanya kazi katika ubalozi wakati huo.

Polisi waliwahi kufika katika eneo la tukio baada ya kupokea simu kutoka kwa mwajiriwa wa bafu hilo. Wakati wa mahojiano, mwanamume huyo aliripotiwa kukiri kuchukua video, lakini alikataa kuambatana kwa hiari na maafisa wa polisi kwenda kituo cha polisi au kukabidhi simu yake, akielezea kinga yake ya kidiplomasia dhidi ya kukamatwa.

Alirejea nchini Singapore mwezi Aprili.

Polisi wa Tokyo walimtaka mwanamume huyo kujisalimisha kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ya Japani mwezi Mei. Aliripotiwa kukubali ombi hilo na kufika Japani mwezi huu.

Wanadiplomasia wana kinga ya kufunguliwa mashtaka kwenye nchi mwenyeji. Polisi wanasema mwanamume huyo hana tena kinga ya kidiplomasia.

Mshauri huyo wa zamani aliripotiwa kuwaambia wanahabari wakati wa mahojiano ya hiari kwamba alichukua video mara kadhaa. Mwanamume huyo alisema alikuja nchini Japani kuelezea majuto yake na kuzungumza kama raia wa kawaida.