NHK WORLD > Ukurasa wa mwanzo wa Idhaa ya Kiswahili > Kuhusu NHK

Kuhusu NHK

NHK ni shirika pekee la utangazaji la umma nchini Japani. Lilianza kurusha matangazo ya redio mwaka 1925. Shirika hili linaendeshwa kwa kupokea michango inayotolewa na kaya zinazomiliki seti za televisheni kwa lengo la kuliwezesha kutoa matangazo bora bila ushawishi wa serikali au mashirika ya binafsi na kuweka umuhimu katika maoni ya wasikilizaji na watazamaji.

NHK hivi sasa linatoa matangazo yake kwa chaneli zipatazo nne za televisheni na tatu za redio za ndani ya nchi. Chaneli ya televisheni ya matangazo ya jumla na ya matangazo ya elimu ni huduma kuu ya matangazo ya nchi nzima. Chaneli tatu za redio za ndani ya nchi zinatoa habari, vipindi vya kuelimisha, burudani za familia, na kadhalika. Chaneli zipatazo mbili za matangazo ya televisheni za setilaiti zinaendesha vipindi vinavyoweza kubadilika ili kukidhi matakwa ya watazamaji wa aina mbalimbali. Vilevile, NHK WORLD inatoa huduma za matangazao ya kimataifa.

Kuhusu NHK WORLD

NHK WORLD ni shirika la utangazaji la kimataifa.
NHK inaendesha idhaa za matangazo ya kimataifa ya televisheni, redio na intaneti. Kwa pamoja zinajulikana kama NHK WORLD.

Malengo ya NHK WORLD

Huduma

“NHK WORLD TV” (Matangazo ya kimataifa ya Televisheni)
NHK WORLD TV ni idhaa ya matangazo ya televisheni kwa lugha ya kiingereza kwa wasikilizaji kote duniani. Hurusha matangazo yake duniani kote kupitia satelaiti tatu za mawasiliano. NHK WORLD TV hutangaza habari za kisasa zaidi kutoka Japani, Asia na duniani kote, ikiwa ni pamoja na uandaaji wa vipindi mbali mbali kwa saa 24.
“NHK WORLD PREMIUM” (Usambazaji wa vipindi)
NHK WORLD PREMIUM hutangaza vipindi saa 24 kwa siku kupitia mitandao ya watoa huduma za matangazo ya televisheni ya kebo na satelaiti katika nchi mbalimbali. Mbali na habari na vipindi arifu vya NHK, idhaa hiyo pia husambaza drama, vipindi vya sanaa, utamaduni, burudani, michezo na vipindi vya watoto.
“NHK WORLD RADIO JAPAN”
NHK WORLD RADIO JAPAN hutangaza dunia nzima katika lugha 18, ikiwa ni pamoja na kiingereza na Kijapani. Idadi ya saa za matangazo katika kila lugha hutofautiana, lakini jumla ya saa 55 na dakika 20 za matangazo hutumika kila siku.
“NHK WORLD INTERNET SERVICE”
Tovuti katika lugha 18 tofauti hutoa habari, vipindi na masomo ya lugha ya kijapani. Tovuti pia hutoa huduma ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na habari kwa video, kwa sauti, habari ya maandishi, huduma ya habari kwa njia ya simu ya mkononi, na huduma ya kujifunza lugha ya kijapani. (tafadhali jua kwamba huduma zinazopatikana hutofautiana kutegemeana na lugha)