NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Misamiati na Majaribio > Orodha ya Misamiati

Orodha ya Misamiati na Majaribio

Somo la 6

電話をします [DENWA O SHIMASU]

Nitakupigia simu.
DENWA ni “simu.” O inaonyesha mtendwa. SHIMASU ni kitenzi kinachomaanisha “kufanya kitu fulani.”
Unaweza kutumia vitenzi vya umbo la MASU kwa ajili ya kuelezea kile unachokifanya wakati huo, lakini pia kile utakachokifanya katika siku za usoni.

Maneno na semi katika somo

さくら ところでアンナさん。
電話番号は何番ですか。
Anna, licha ya hivyo, namba yako ya simu ni ipi?
Sakura TOKORODE ANNA-SAN. DENWABANGÔ WA NANBAN DESU KA.
Anna, licha ya hivyo, namba yako ya simu ni ipi?
アンナ ええと。080-1234-・・・。 Ee.... 080 – 1234 – ....
Anna ÊTO. REI HACHI REI - ICHI NI SAN YON - ...
Ee.... 080 – 1234 – ....
さくら ありがとう。
じゃ、今度、電話をしますね。
Asante. Basi, nitakupigia wakati mwingine.
Sakura ARIGATÔ. JA, KONDO, DENWA O SHIMASU NE.
Asante. Basi, nitakupigia wakati mwingine.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.