Orodha ya Misamiati na Majaribio
Somo la 1
よろしくお願いします [YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU]
Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
Unapojitambulisha kwa mtu unasema YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU. Katika muktadha huu ikimaanisha, "Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa." Pia unaweza kutumia usemi huo kama ishara ya kukamilisha mazungumzo wakati ambapo unamuomba mtu akufanyie jambo fulani.
Maneno na semi katika somo
アンナ | はじめまして。私はアンナです。 | Nashukuru kukutana nawe. Mimi ni Anna. |
---|---|---|
Anna | HAJIMEMASHITE. WATASHI WA ANNA DESU. Nashukuru kukutana nawe. Mimi ni Anna.
|
|
さくら | はじめまして。さくらです。 | Nami pia. Mimi ni Sakura. |
Sakura | HAJIMEMASHITE. SAKURA DESU. Nami pia. Mimi ni Sakura.
|
|
アンナ | よろしくお願いします。 | Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
|
Anna | YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU.
Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
|
|
さくら | こちらこそ。 | Ni mimi ninayestahili kusema hivyo.
|
Sakura | KOCHIRAKOSO.
Ni mimi ninayestahili kusema hivyo.
|