NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Kujifunza Kijapani kwa mtandao > Vidokezo kuhusu Japani
Vidokezo kuhusu Japani
Soma kwa muhtasari utamaduni, mila, lugha na adabu za Kijapani. Huenda ukakutana na kitu ulichokitamani sana.
Somo la 50Sasete itadakimasu
Katika mazungumzo ya kisasa kati ya Wajapani kunatokea ~SASETE ITADAKIMASU mara nyingi. Tunaona wamezidi wanaofikiria kuwa wakisema ~SASETE ITADAKIMASU, basi wanaweza kutoa heshima kwa neno hilo tu.
Mathalani, mwanzo wa mkutano, watu hao wanawaambia waliohudhuria SETSUMEI SASETE ITADAKIMASU, 'Ningependa kueleza.' Kwa hapa tunaona, SETSUMEI SHIMASU, 'Nitaeleza,' inatosha.
Aidha, unaweza kuona mlango wa duka fulani umeandikwa JÛJI KARA EIGYÔ SASETE ITADAKIMASU, 'Tungependa kufungua kuanzia saa nne.' Hayo ni matumizi yasiyo sahihi.
Lakini, lugha hubadilika na wakati. Mwishowe semi kama hizo huenda zikawa 'Kijapani sahihi'.
Somo la 49Kuoga
Nchini Japani takriban kila nyumba ina bafu lake. Ukubwa wake ni kama mwanamume mtu mzima anaweza kukaa kitako ndani na miguu ameinyoosha na maji yanafika hadi mabegani. Maji yamoto bafuni yanatumiwa na wote nyumbani, hivyo, unasafisha kichwa na mwili kabla ya kuingia bafuni.
Wajapani si wanaoga nyumbani tu, bali wanakwenda sana pahali pa chemchemi ya maji yamoto pia. Safari ya kwenda kuoga chemchemi ya maji yamoto inaitwa ONSEN RYOKÔ. Baadhi ya hoteli za chemchemi za maji yamoto zina mabafu yanayoitwa ROTENBURO, mabafu ya nje.
Somo la 48Vyakula vya msimu hasa
Nchini Japani kuna majira manne, na kila majira yana vyakula vyake vya msimu hasa. Tufahamishe vitu kadha vya kula vya msimu hasa.
Majira ya chipukizi, vinavyowakilisha majira ni 'chipukizi za mianzi', na 'zunuba wa kwanza', yaani aina moja ya samaki wa baharini ambao wanauzwa katika mwanzo mwanzo wa msimu wake hasa.
Majira ya joto, yaani kiangazi, tunakula 'matango', 'mikunga' na kadhalika. Matango yanapoza miili iliyopata hari au joto, na yanatumika sana kuwa ni mboga ya kuzuia machofu ya kiangazi.
Majira ya pukutizi yana vitu vingi vinakaribisha msimu wake hata yaitwe 'majira ya hamu ya kula'. Kuna 'KAKIi', inayofanana na tini, 'SAMMA', aina ya samaki mwembamba kama kisu, 'uyoga' na kadhalika.
Majira ya baridi tunakula sana 'figili', 'TARA', aina ya chewa, na kadhalika.
Kwa kuwa vitu vya kula vya msimu hasa vinatolewa masokoni kwa wingi, huwa ni rahisi, hivyo ni rafiki wa watu wa kawaida. Hasa, riziki za baharini vitu vya msimu wake hasa vinathaminiwa, kwa mfano, watu wanafurahi kuonja na huku wakipiga kelele, 'Zunuba wa kwanza wa mwaka huu!'.
Somo la 47Mazao mahsusi
Jinsi visiwa vya Japani vilivyoenea kwa urefu kutoka kaskazini kwenda kusini hali ya hewa hubadilika sehemu hata sehemu na kuonyesha majira manne yenye utajiri. Kila sehemu nchini Japani ina mazao yake mahsusi.
Shizuoka iliyo chini ya mlima wa Fuji mazao yake mahsusi ni majani ya chai, na inajisifu idadi ya uzalishaji majani ya chai ya nafasi ya kwanza nchini Japani. Aidha Shizuoka imekabiliana na bahari hata ikabarikiwa kwa mazao ya baharini pia kama vile SHIRASU, aina ya dagaa wadogo, SAKURAEBI, aina ya uduvi, na kadhalika.
Bila shaka, hata Tokyo ina mazao yake mahsusi, nayo ni NORI, ambayo haikosekani kwa SUSHI, na asili yake ni mwani wa baharini. Inayopatikana katika Ghuba ya Tokyo imepata sifa nzuri kwa sababu ina kiasi kikubwa cha utamu na harufu.
Siku hizi, ukitumia huduma ya kuagiza kwa kupitia mtandao wa intaneti, basi utaweza kupata mazao mahsusi kutoka kokote nchini na kujifurahisha nayo. Lakini ni anasa ya mwisho kutembelea pahali penyewe ukaonja ladha ya msimu hasa, au siyo?
Somo la 46Mlima wa Fuji
Majira mwafaka ya kupanda mlima wa Fuji ni miezi ya Julai na Agosti. Kwa muda wa miezi hii miwili, watu wasiopungua laki tatu wanakusudia kufika kileleni. Karibu asilimia 30 kati yao ni watu wa nchi za nje. Ingawa miezi hiyo imo katika kiangazi, lakini halijoto inashuka ghafla na hali ya hewa huwa rahisi kubadilika ukikaribia kilele chenye urefu wa mita 3776 kutoka usawa wa bahari. Mavazi ya mvua na ya kuzuilia baridi, maji ya kunywa, na chakula cha dharura ni mahitaji yasiyokosekana. Na tena ni lazima kuchukua hadhari na ugonjwa wa urefu mkubwa.
Ijapokuwa mlima wa Fuji unapendwa na watu wa jinsia zote mbili, lakini ulikuwa hauruhusiwi kupandwa na wanawake hadi miaka 150 hivi iliyopita. Juu ya hivyo, kumebakia maandishi kwamba baadhi ya wanawake waliovalia kiume walipanda na hali wamechanganyika na wanaume hata kabla ya hapo. Tunaona kilele cha mlima wa Fuji kimekuwa kinavutia nyoyo za watu toka zamani za kale.
Makala mpya
Kuangalia
RSS
Kuangalia zaidi
Bookmark
![[Bure] Kutafuta na kuhifadhi masomo (Sauti /Maandishi)](../images/btn_dl.png)