NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Kujifunza Kijapani kwa mtandao > Vidokezo kuhusu Japani

Vidokezo kuhusu Japani

Soma kwa muhtasari utamaduni, mila, lugha na adabu za Kijapani. Huenda ukakutana na kitu ulichokitamani sana.

Somo la 35Jumuia ya mtaa

Jumuia ya mtaa ni chombo ambacho wakaazi wa sehemu moja mjini au kijijini wanafanya mtaa wao uwe mzuri wa kuishi. Inaitwa CHÔNAI-KAI au JICHI-KAI. Moja kati ya harakati zake kubwa ni usafishaji uliotokea katika mazungumzo ya leo. Aidha, wanafanya na kutekeleza mipango kama vile sherehe ya kiangazi, tamasha ya fashifashi, na nyingine ili wakaazi wapate hisia ya umoja. Isitoshe, wanafanya mzunguko mtaani kwa ajili ya kuzuia uhalifu, na wanafanya mazoezi ya kuzuia maafa dhidi ya mtetemeko mkubwa wa ardhi.

Kuangalia somo la 35

Somo la 34Kuchanganyika na majirani

Kila taifa lina desturi yake. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mkoa fulani ambao watu wa kigeni wanazidi ghafla hivi karibuni, walipata matokeo kwamba matatizo yanayohusika na utoaji takataka na makelele yanazidi. Hasa, mwainisho wa takataka hauachi kuyasababisha matatizo hata kati ya Wajapani pia kwa sababu namna ya kuainisha na siku za kukusanya zinatofautiana sehemu hata sehemu. Serikali za miji au vijiji ambazo zina watu wa kigeni wengi zinaeleza namna ya kuainisha takataka kwa lugha za kigeni na kusambaza mabango yenye picha. Tujitahidi kujenga uhusiano mzuri na majirani kwa kutoa takataka kwa namna ipasayo bila ya kusema 'Ni balaa ...', wala 'Ikiwa mimi peke yangu ...' 'Huenda ikawa ni takataka tu, hata hivyo ni takataka.'

Kuangalia somo la 34

Somo la 33Misemo inayolainisha mawasiliano

Nchini Japani fikra ya kuwa 'WA ndio unaoheshimiwa kabisa' inaishi hata katika dunia ya biashara. Dhana hiyo ya 'WA' ni usanisia au jumlisho la maana kama hizi: amani, upole, utulivu, ushirikiano, na utegemeano. Msemo unaoashiria moyo wake vizuri ni O-KAGE SAMA DE, 'kwa msaada wenu'. Unaweza kutumia kama vile 'Nimepata mkataba kwa msaada wenu.' Hata ikiwa ulifanikiwa kufanya kazi hiyo kama ni kiini, unatamka namna unavyoheshimu ushirikiano kwa kusema O-KAGE SAMA DE iliyotiwa hisia kuwa 'mafanikio ni matokeo ya maelekezo na misaada kutokana na watu mbali mbali'. Aidha, ukianzia ZANNEN NAGARA..., 'Nasikitika ...', inafahamika kuwa ni habari mbaya. OSSHARU TÔRI DESU GA..., 'Hivyo ndivyo unavyosema, lakini ...' inakupa uanze maoni yako pamoja na kivuli cha maana ya 'Ninafahamu unalotaka kulisema, lakini...'. Ukimudu kutumia semi namna hizi kama unavyotaka, basi unafikiriwa ni mwanajamii mtu mzima.

Kuangalia somo la 33

Somo la 32Unasemaje ukapanga?

Kampuni zinazoajiri watu wa nchi za nje zina programu za kuwafundisha adabu za biashara za kipekee za Kijapani na matumizi ya lugha. Juu ya hivyo, 'utata' ambao ni sifa moja ya lugha ya Kijapani unaweza kusababisha matatizo yasiyofikirika.
Mathalani, mkubwa wa sehemu fulani ya kampuni alimwambia mtu wake wa kigeni aliyeweka vitu ovyo mezani kwamba "KIREI NI SHITARA?". Lakini siku ya pili yake, mezani hakukusafika kamwe. Ingawa alikusudia kumwelekeza 'apange vitu mezani mara moja,' lakini inaonekana hakufanikiwa kuwasilisha nia yake hasa. "KIREI NI SHITARA?"maana yake neno kwa neno ni 'Naona itakuwa vizuri kama ukipanga sawa'. Kwa upande mwingine, mdogo wake alichukulia nasaha tu, asifanye chochote. Mkubwa wake naye ilikuwa lazima amuelekeze kwa hakika kama asiweke kitu mezani isipokuwa kompyuta tu. Juu ya hivyo, ni mbinu ya kufanya kazi nchini Japani kufahamu maana sawa hata kama ni maelekezo yenye utata.

Kuangalia somo la 32

Somo la 31Treni ya kwenda na kurudi kazini

Wajapani wanatumiaje wakati ndani ya treni huku wakienda kazini asubuhi na kurudi nyumbani jioni?
Kwa mujibu wa utafiti wa hojaji uliofanywa na kampuni binafsi ya utafiti, kati ya mambo wanayoyafanya wanaume, jambo la kwanza, yaani jambo wanalolifanya wengi zaidi, nalo ni kusoma vitabu vilivyokuwa pamoja na katuni, na la pili ni kusoma matangazo yaliyobandikwa ndani ya treni, likifuatwa na kuangalia mandhari nje ya treni, na kufikiria la kufikiria. Kwa upande wa wanawake, la kwanza ni kupelekeana baruapepe na kucheza michezo kwa kutumia simu ya mkononi, la pili, kusoma vitabu, na la tatu, kusikiliza muziki. Aidha, waliojibu "wanasinzia" ni wengi kiasi kwa jinsia zote mbili. Kwa upande mwingine, takriban hakuna mtu aliyejibu "kupiga gumzo na mtu".
Katika treni ya kwenda na kurudi kazini, si nadra kutokuwa na sauti ya mtu kabisa isipokuwa matangazo yake. Mtu au watu waliokuja Japani kutoka nchi za nje ambako mazungumzo yanaanza yenyewe kati ya waliosadifu kuwemo ndani ya treni moja, nao watashangaa juu ya hali ya ukimya ndani ya treni. Lakini "Ukiwa Urumi tenda kama Warumi." Ukianza kusema ghafla kwa simu yako ya mkononi katika treni iliyojaa watu, utakodolewa macho makavu mara moja.

Chanzo; Kampuni ya L-NET

Kuangalia somo la 31

[Bure] Kutafuta na kuhifadhi masomo (Sauti /Maandishi)

Kwa maswali au maoni kuhusu Jifunze Kijapani: Kutuma maoni