NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Nafikiri kwamba (Somo la 39)

Mwalimu Tufundishe

Nafikiri kwamba (Somo la 39)

Unapoelezea fikra, maoni au makisio yako, kwanza unasema kile unachofikiria, na kisha unasema TO OMOIMASU, (Nafikiri kwamba). OMOIMASU ni kitenzi kinachomaanisha (kufikiri). Unaongeza TO baada ya kile unachofikiria.

Kabla ya TO OMOIMASU (Nafikiri kwamba), unatumia muundo wa kawaida wa kitenzi, kama vile umbo la kikamusi au umbo la TA la vitenzi.
Katika somo la 26 ulijifunza kuhusu vitenzi vya muundo wa kawaida.

Kwa mfano, tutengeneze sentensi inayomaanisha “Nafikiri atakuja.” KANOJO inaonyesha mwanamke. “Kuja,” unatumia umbo la kikamusi la kitenzi, KURU. Kwa hiyo unasema, KANOJO WA KURU (atakuja). Baada ya hapo utaongeza TO OMOIMASU (Nafikiri kwamba). Kwa pamoja unasema KANOJO WA KURU TO OMOIMASU (Nafikiri atakuja). Ikiwa vivumishi vya I vinakuja kabla ya TO OMOIMASU, vivumishi havibadiliki. Je, unasemaje kwa Kijapani “Nafikiri ni mrembo”?
“Mrembo ” ni UTSUKUSHII, ikiwa ni kivumishi cha I.
Kwa hiyo jibu ni KANOJO WA UTSUKUSHII TO OMOIMASU.

Ikiwa nomino au vivumishi vya NA vinakuja kabla ya TO OMOIMASU, unachotakiwa kufanya ni kusema DA baada ya neno hilo.
Je, unasemaje “Nafikiri hiyo inafaa” kwa Kijapani?
“Hiyo” ni SORE. “inafaa” ni BENRI ambayo ni kivumishi cha NA. Hivyo unaweka DA baada ya kivumishi hicho, na useme BENRI DA. Kisha itakuwa SORE WA BENRI DA (hiyo inafaa). Baada ya hapo, unaongeza TO MOIMASU (Nafikiri kwamba).
Kwa pamoja, unasema SORE WA BENRI DA TO OMOIMASU (Nafikiri inafaa).
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.