NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Tofauti kati ya KARA na NODE (Somo la 28)

Mwalimu Tufundishe

Tofauti kati ya KARA na NODE (Somo la 28)

KARA na NODE huelezea sababu. Kwa mfano, ikiwa kivumishi, KAWAII, (kupendeza), ndio sababu, unaweza kusema ama KAWAII KARA au KAWAII NODE. Lakini unapoyatumia na kivumishi cha NA au nomino, KARA huwa DAKARA, na NODE inabadilika na kuwa NANODE. Kwa mfano, YAKUSOKU (ahadi), ndio sababu. YAKUSOKU ni nomino. Kwa hiyo ikiwa utatumia KARA, unasema YAKUSOKU DAKARA. Ikiwa unatumia NODE, unasema YAKUSOKU NANODE.
KARA na NODE kwa karibu zinamaanisha kitu kimoja. Lakini ukitumia NODE, maelezo yako yatasikika kwa upole. Kwa sababu N inayotokana na NODE inasikika kwa upole zaidi kuliko K inayopatikana kwa KARA. Kwa hiyo, NODE, mara nyingi hutumika kwenye biashara na katika matukio rasmi. Watu wanataka kusikika kiungwana na kwa upole zaidi wakati kama huo.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.