NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kauli ya kutendewa (Somo la 23)

Mwalimu Tufundishe

Kauli ya kutendewa (Somo la 23)

Unatumia umbo la kutendewa, ikiwa unazungumza kwa mtazamo wa mtu aliyetendewa jambo. Ili kufanya hivyo, unatumia kitenzi cha umbo la kutendewa na uelezee ni nani aliyetenda kitendo hicho kwa kutumia NI. 
Sasa, hebu nikuelezee namna ya kunyambua vitenzi vya umbo la MASU hadi umbo la kutendewa. Kwanza ni kuhusu vitenzi ambavyo irabu zake kwenye silabi za kabla tu ya MASU vinamalizikia na "E." Hapa, kabla ya MASU, unaweka RARE. Kwa hiyo, TABEMASU (kula) inageuka na kuwa TABERAREMASU (kuliwa).

Pili ni kuhusu vitenzi ambavyo irabu zake kwenye silabi kabla tu ya MASU ni "I." Kwa vitenzi kama hivi, kuna namna mbili. Namna ya kwanza ni kubadilisha irabu "I" na kuwa" A." Kisha, unaongeza RE, na kusema MASU. Katika muktadha huu, SHIKARIMASU (kukaripia), unabadilisha RI kabla ya MASU na kuwa RA na uongeze RE. Kwa hiyo inakuwa SHIKARAREMASU (kukaripiwa). SHIMASU (kufanya), katika umbo la kutendewa inakuwa SAREMASU.
Namna ya pili ni kupachika RARE kabla ya MASU. MIMASU (kuangalia) inageuka na kuwa MIRAREMASU, (kuangaliwa).
Na mwisho, nikufahamishe kitenzi ambacho kinanyambulika katika namna isiyokuwa ya kawaida.
KIMASU (kuja) inageuka na kuwa KORAREMASU.
Nenda ukurasa wa "Nyenzo za kujifunzia."
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.