NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Vitenzi vya umbo la NAI (Somo la 21)

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la NAI (Somo la 21)

Vitenzi vinavyomalizikia na NAI, vinaitwa "vitenzi vya umbo la NAI."
Nitakuelezea namna ya kubadilisha vitenzi vya umbo la MASU na kuwa umbo la NAI. Yaani kubadilisha vitenzi vya umbo la MASU na kuwa katika hali ya kawaida ya kukanusha ya umbo la NAI. Kwanza, ikiwa irabu kwenye silabi kabla tu ya MASU inamalizikia na "E," unachohitajika kufanya ni kubadilisha MASU na kuwa NAI. Kwa mfano, TABEMASU (ninakula) inageuka na kuwa TABENAI (sili).

Sasa, ikiwa irabu ya silabi kabla tu ya MASU inaishia na " I," kuna namna mbili.

Namna ya kwanza, unabadilisha MASU na kuwa NAI. Kwa mfano, OKIMASU (naamka), inageuka na kuwa OKINAI (siamki). Katika namna ya pili, unaondoa neno MASU, halafu ubadilishe irabu ya silabi kabla tu ya MASU na kuwa "A," na uongeze NAI.
Acha nikuelezee hili na IKIMASU (ninaenda), kama mfano. Hapa, silabi kabla ya MASU ni KI. Kwanza unabadilisha KI na kuwa KA, halafu uongeze NAI. Kwa hiyo umbo la NAI la IKIMASU ni IKANAI (siendi).

Lakini ukiondoa MASU, ikiwa silabi iliyopo kabla tu ya neno hilo ni irabu "I" peke yake bila konsonati, unabadilisha "I" na kuwa WA, halafu unaongeza NAI. Kwa hiyo, TSUKAIMASU (ninatumia) inageuka na kuwa TSUKAWANAI (sutumii).

Na mwisho, nikufahamishe kitenzi ambacho kinanyambulika katika namna isiyokuwa ya kawaida.
KIMASU (ninakuja) inageuka na kuwa KONAI (siji).
Tafadhali angalia ukurasa wa "Nyenzo za kujifunzia."
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.