NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Mfumo wa uandishi wa Kijapani (Somo la 1)

Mwalimu Tufundishe

Mfumo wa uandishi wa Kijapani (Somo la 1)

Lugha ya Kijapani ina aina tatu ya mfumo wa herufi, kila moja ikiwa na jukumu lake. Unapoandika WATASHI WA ANNA DESU (Mimi ni Anna), nomino ya kujitambulisha yaani "mimi," WATASHI, inaandikwa kwa herufi ya Kanji. WA, DESU na maneno mengine yanayoonyesha matumizi ya kisarufi, yanaandikwa kwa herufi za Hiragana. Vitenzi na vivumishi vinaandikwa kwa herufi za Kanji na Hiragana kwa pamoja. Majina ya kigeni na maneno ya mkopo, yaani maneno ambayo chanzo chake ni lugha za kigeni, kama vile “Anna", yanaandikwa kwa herufi za Katakana.

Hiragana na Katakana ni alama za fonetiki, kila moja ikiwakilisha silabi moja. Lugha ya Kijapani ina irabu tano: a, i, u, e, o. Na ina konsonanti tisa. Kwa Kijapani kila irabu, ama konsonanti na irabu huunda silabi moja. Zaidi ya hayo, kuna "n."

Jaribu kuandika jina lako kwa Kijapani, ukizingatia mfumo wa maandishi uliopo kwenye jedwali linalopatikana kwenye kitabu cha kiada cha kipindi hiki, au kwenye tovuti hii.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.