NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > "Jifunze Kijapani" ni nini?

"Jifunze Kijapani" ni nini?

Masomo ya sarufi (Toleo la 2015)

  • Maizi sarufi ya msingi!
  • Tanakali sauti za kufurahisha zinapatikana.
"Jifunze Kijapani" ni nini?

"Jifunze Kijapani"ni kipindi cha kujifunza lugha ya Kijapani kinachoandaliwa na Shirika la utangazaji la umma nchini Japani, NHK WOLRD-JAPAN. Unaweza kujifunza sarufi za msingi na misemo muhimu. Unaweza kupakua maandiko ya masomo.

Utangulizi wa simulizi

Mhusika mkuu wa simulizi hii ni Anna, mwanafunzi kutoka Thailand aliye na umri wa miaka 20 ambaye anapenda katuni za Kijapani za manga. Amekuja nchini Japani kujifunza lugha ya Kijapani kwa mwaka mmoja kwenye chuo kikuu kimoja jijini Tokyo. Atajifunza Kijapani kinachotumika katika maisha ya kawaida kupitia tajriba mbalimbali, kama vile masomo ya chuoni, maisha yake ya kila siku bwenini, katika manunuzi na safarini.

Wahusika wakuu

Anna

Mwanafunzi kutoka Thailand. Anapenda katuni za Kijapani za manga, na lengo lake ni kuwa na uwezo wa kusoma maandishi ya Kijapani ya katuni za manga bila matatizo yoyote. Yeye ni mchangamfu na ana shauku kubwa. Hata kwa kufanya makosa wakati fulani, anajifundisha lugha ya Kijapani, desturi na hatimaye anajiimarisha zaidi.

Sakura

Sakura ni mwanafunzi kwenye chuo kikuu anachosomea Anna. Anasoma akiwa na nia ya kutaka kuwa mwalimu atakayefundisha lugha ya Kijapani. Yeye ni mwelekezi anayewasaidia wanafunzi wa kigeni na anamsaidia Anna aweze kuzoea maisha ya Japani. Anatoka mkoa wa Shizuoka ulioko pwani ya Pasifik.

Rodrigo

Rodrigo ni mwanafunzi kutoka Mexico na ni mwanafunzi mwenza wa Anna. Yeye ana shauku ya kujua historia ya Japani. Ana ufahamu na ni mkweli, lakini wakati mwingine ni mchangamfu.

Prof. Suzuki

Profesa Suzuki anamfundisha Anna na wanafunzi wengine wa kigeni lugha ya Kijapani. Yeye ni mwalimu wa kutegemewa. Pia huwapatia ushauri wanafunzi wanapokuwa na matatizo.

Mama msimamizi wa Bweni

Ni mama anayesimamia bweni analoishi Anna. Anapendwa sana na wanafunzi ambao wanamuita "Okâsan", neno la Kijapani linalomaanisha "mama". Ni mkali lakini anawaangalia vizuri wanafunzi kutoka nchi zingine.

Kenta

Kenta ni binamu yake Sakura. Ni mwanafunzi wa chuo kikuu, anayeishi katika mkoa wa Shizuoka, mji anakotokea Sakura. Chuoni anashiriki katika kilabu ya upigaji picha.

Msimamizi wa Masomo

Akane Tokunaga

Akane Tokunaga

Profesa Mshiriki – Chuo Kikuu cha Kanda cha masomo ya kimataifa

Tokunaga amekuwa akishiriki katika shughuli mbalimbali kama mwalimu wa Kijapani tangu miaka ya 1990. Kuanzia mwaka 2000, amekuwa akiwafundisha wanafunzi wa kigeni somo la utamaduni na lugha ya Kijapani katika chuo kikuu cha Kanda cha masomo ya kimataifa. Pia amehusika kwenye utengenezaji wa nyenzo za kufundishia. Tokunaga anaheshimika kwa masomo yake ya vitendo.