NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 35

Somo la 35

Naweza kutumia kadi ya kufanyia manunuzi?

Anna pamoja na Kenta, walifurahia mlo wa sushi katika mgahawa wenye mikanda ya kubebea chakula.

Somo la 35 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

KUREJITTO KÂDO WA TSUKAEMASU KA

Mazungumzo

健太 お勘定をお願いします。 Naweza kupata bili yangu, tafadhali?
Kenta OKANJÔ O ONEGAI SHIMASU.
Naweza kupata bili yangu, tafadhali?
店員 全部で5200円です。 Kwa jumla, ni yeni 5,200.
Muuzaji ZENBU DE GOSEN NIHYAKU EN DESU.
Kwa jumla, ni yeni 5,200.
健太 クレジットカードは使えますか。 Naweza kutumia kadi ya kufanyia manunuzi?
Kenta KUREJITTO KÂDO WA TSUKAEMASU KA.
Naweza kutumia kadi ya kufanyia manunuzi?
店員 はい、使えます。 Ndiyo, unaweza kutumia.
Muuzaji HAI, TSUKAEMASU.
Ndiyo, unaweza kutumia.

Vidokezo vya sarufi

Namba (3)

Tujifunze namba kubwa.
Tafadhali tembelea ukurasa wa nyezo za kujifunzia.

Mwalimu Tufundishe

Umbo la uwezekano la vitenzi
Umbo la uwezekano la vitenzi huwa na maana mbili.

Tanakali Sauti

Sauti za elektroni
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kenta alinipeleka nikale sushi! Unasema GOCHISÔSAMA DESHITA baada ya kula. Pia nimejifunza ya kwamba unasema GOCHISÔSAMA DESHITA, kwa mtu aliyekulipia chakula.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.