NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 30

Somo la 30

Ningependa kupiga picha zaidi kidogo.

Anna alipokuwa akipiga picha za Mlima Fuji akiwa na Sakura na Kenta kukaanza kunyesha.

Somo la 30 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

MÔ SUKOSHI SHASHIN O TORITAI DESU

Mazungumzo

さくら あ、雨だ。急いで帰りましょう。 Ah! Mvua imeanza kunyesha. Turudi haraka.
Sakura A, AME DA. ISOIDE KAERIMASHÔ.
Ah! Mvua imeanza kunyesha. Turudi haraka.
アンナ ちょっと待ってください。もう少し写真を撮りたいです。 Subiri kidogo, tafadhali. Ningependa kupiga picha zaidi kidogo.
Anna CHOTTO MATTE KUDASAI. MÔ SUKOSHI SHASHIN O TORITAI DESU.
Subiri kidogo, tafadhali. Ningependa kupiga picha zaidi kidogo.
健太 雨にぬれたら、風邪をひくよ。 Ikiwa utanyeshewa, unaweza kupata homa.
Kenta AME NI NURETARA, KAZE O HIKU YO.
Ikiwa utanyeshewa, unaweza kupata homa.

Vidokezo vya sarufi

  TAI DESU

Kwa kubadilisha sehemu ya MASU ya vitenzi vya umbo la  MASU kuwa TAI, unaweza kuelezea kile unachotaka kufanya.  
Ikiwa utaongeza DESU baada ya TAI, sentensi itakuwa ya kiungwana.

k.m.) SHASHIN O TORIMASU
(Napiga picha.)
>> SHASHIN O TORITAI DESU
(Nataka kupiga picha.)

Mwalimu Tufundishe

Tofauti kati ya TARA na TO
TARA na TO zote mbili zinaonyesha sharti. Ikiwa kitu kitatokea kutokana na sharti fulani, unatumia TARA au TO kuashiria sharti hilo.

Tanakali Sauti

Radi / Kuviringika
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

“Nimesikia ya kwamba kuna misemo mingi nchini Japani inayoangazia hali ya hewa. Mifano ikiwa kunapendeza wakati wa machweo, siku inayofuata hali ya hewa itakuwa nzuri. Au ikiwa kuna upinde wa mvua asubuhi, kutanyesha.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.