NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Kujifunza Kijapani kwa mtandao > Somo la 3 Ndiyo, nimeelewa.

Kujifunza Kijapani kwa mtandao Somo la 3 Ndiyo, nimeelewa.

Mkubwa wa Bw. Kuon, Bi. Yamada alipohakikisha ratiba ya leo, alikumbukia kuna mpango muhimu!

Anzisha sauti fungua ukurasa mpya

Kutafuta na kuhifadhi maandishi ya masomo yote 50 (PDF)

Misemo muhimu: HAI, WAKARIMASHITA

Mazungumzo kwa undani
山田クオンさん、ちょっと…。
Hebu, Kuon san.
YAMADAKUON-SAN, CHOTTO...
クオンはい。
Naam.
KUONHAI.
山田今日、これから会議があります。
出て下さい。
Leo kutakuwa na mkutano baadaye.
Tafadhali, hudhuria.
YAMADAKYÔ, KOREKARA KAIGI GA ARIMASU.
DETE KUDASAI.
クオンはい、わかりました。
場所はどこですか?
Ndiyo, nimeelewa.
Mahali ni wapi?
KUON HAI, WAKARIMASHITA.
BASHO WA DOKO DESU KA?

Vidokezo kuhusu Japani (じょうたつのコツ)

Wajapani tunaheshimu ‘uelewano’ katika uhusiano kati ya watu. Kwa hivyo, hatupendi kuwa uhusiano unakuwa mbaya kwa sababu ya kukataa waziwazi. Kwa mfano, wakati wa kukaribishwa chakula usichokipenda, kwanza unasema ARIGATÔ
GOZAIMASU kushukuru kwa kukaribishwa. Na wakati wa kukataa ushawishi, unaweza kusema CHOTTO... na kukokoteza jawabu. CHOTTO hii inatumika sana si unapomsemesha mtu tu bali unapotaka kukataa pia. Na tasifida au usafidi pia unatumika sana katika mandhari ya biashara. Usemi unaotumika sana kukataa shauri ya biashara ni KENTÔ
SHITEMIMASU. KENTÔ SHITEMIMASU maana yake ni ‘nitazidi kuzingatia’, lakini ukweli wa mambo ina maana nyingine ya ‘usitarajie jibu zuri’ ndani yake.

« Somo lililopitan (2)  |  Somo linalofuata (4) »

Kurudi orodha ya masomo

Orodha ya masomo:Kuongezwa kila wiki

Utambulisho

Kujipima

Kutafuta kwa kutumia mada

  • Ushauri, maoni na maombi
  • Kuomba muongozo na maelezo
  • Misemo inayotumika sana
  • Kuelezea hali halisi
  • Kutoa maoni
  • Kusalimiana
  • Misemo ya adabu
  • Kujibu
  • Kujitambulisha
  • Kufanya manunuzi
[Bure] Kutafuta na kuhifadhi masomo (Sauti /Maandishi)

Kwa maswali au maoni kuhusu Jifunze Kijapani: Kutuma maoni