NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 29

Somo la 29

Tukiangalia kwa karibu, unaonekana mkubwa, au siyo?

Anna ametembelea mji wa Shizuoka. Leo amepelekwa katika eneo mwafaka la kuutazama mlima Fuji pamoja na Kenta.

Somo la 29 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

CHIKAKU DE MIRU TO, ÔKII DESU NE

Mazungumzo

アンナ 富士山だ。
近くで見ると、大きいですね。
Mlima Fuji.
Tukiangalia kwa karibu, unaonekana mkubwa, au siyo?
Anna FUJISAN DA. CHIKAKU DE MIRU TO, ÔKII DESU NE.
Mlima Fuji. Tukiangalia kwa karibu, unaonekana mkubwa, au siyo?
アンナ あれ。雲の形が帽子みたいです。 Eh! Umbo la wingu linaonekana kama kofia.
Anna ARE. KUMO NO KATACHI GA BÔSHI MITAI DESU.
Eh! Umbo la wingu linaonekana kama kofia.
健太 あの雲が見えると、雨が降るんだよ。 Ikiwa wingu lile litaonekana, mvua itanyesha.
Kenta ANO KUMO GA MIERU TO, AME GA FURU N DA YO.
Ikiwa wingu lile litaonekana, mvua itanyesha.

Vidokezo vya sarufi

  TO

Ikiwa TO inajitokeza baada ya kitenzi, inaashiria sharti la kufanyika jambo fulani. Vitenzi huchukua umbo la kikamusi au la NAI kabla ya TO.
k.m.) ANO KUMO GA MIERU TO, AME GA FURIMASU.
(Ikiwa wingu lile litaonekana, mvua itanyesha.)

Mwalimu Tufundishe

N DA: kauli unayoitumia kuelezea kitu fulani
Umbo la msingi la N DA ni NO DA. Unasema

Tanakali Sauti

Mvua
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Mlima Fuji, ukiwa na mawingu juu yake, pia ni mzuri. Kenta anaweza kutabiri hali ya hewa kutokana na umbo la wingu. Anafahamu mengi. Ni mtu unayeweza kumtegemea.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.