Somo la 22
Nimechelewa.
Anna alifurahia katika kibanda cha Karaoke na rafiki zake kiasi kwamba alirejea bwenini akiwa amechelewa.
Usemi wa msingi:
OSOKU NARIMASHITA
Mazungumzo
アンナ | お母さん、ごめんなさい。遅くなりました。 | Mama, samahani. Nimechelewa.
|
---|---|---|
Anna | OKÂSAN, GOMENNASAI. OSOKU NARIMASHITA.
Mama, samahani. Nimechelewa.
|
|
寮母 | アンナさん、10分も遅刻です。 約束を破ってはいけません。 |
Anna, umechelewa kwa dakika 10. Usivunje ahadi. |
Msimamizi wa bweni | ANNA-SAN, JIPPUN MO CHIKOKU DESU. YAKUSOKU O YABUTTE WA IKEMASEN. Anna, umechelewa kwa dakika 10.
Usivunje ahadi.
|
|
アンナ | すみません。気をつけます。 | Samahani. Nitakuwa mwangalifu.
|
Anna | SUMIMASEN. KI O TSUKEMASU.
Samahani. Nitakuwa mwangalifu.
|
Vidokezo vya sarufi
FUN / PUN: kiambishi cha kutaja dakika
dakika 2 = NIFUN
dakika 10 = JIPPUN / JUPPUN
Ukitaka kujifunza namna ya kutaja dakika 1 hadi 10, nenda ukurasa wa "Nyenzo za kujifunzia."
Umbo la TE la kitenzi + WA IKEMASEN
Ukitumia kitenzi cha umbo la TE na kuongeza WA IKEMASEN, utamaanisha "Usifanye hivyo."
k.m.)
YAKUSOKU O YABUTTE WA IKEMASEN.
(Usivunje ahadi.)
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kubadilisha vivumishi kuwa vielezi
Vivumishi vya Kijapani vinanyambulika na kuwa vielezi.
Tanakali Sauti
Hasira
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Nimemtia wasiwasi sana mama msimazi wa bweni. Nimejifunza ya kwamba ikiwa nitachelewa, Ninastahili kutoa taarifa mapema.