NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 21

Somo la 21

Hapana, siyo sana.

Katika kibanda cha Karaoke, Anna ameimba wimbo wa Kijapani. Sakura anamsifu Anna kwa uimbaji wake mzuri.

Somo la 21 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

IIE, SOREHODODEMO

Mazungumzo

さくら アンナ、上手だね。 Anna, unaimba vizuri.
Sakura ANNA, JÔZU DA NE.
Anna, unaimba vizuri.
アンナ いいえ、それほどでも。 Hapana, siyo sana.
Anna IIE, SOREHODODEMO.
Hapana, siyo sana.
ロドリゴ あっ、もうこんな時間です。 Ah! Muda umekwenda.
Rodrigo A', MÔ KONNA JIKAN DESU.
Ah! Muda umekwenda.
アンナ 大変。門限に間に合わない。 Lo! Sitaweza kuwahi muda wa ukomo wa kurudi.
Anna TAIHEN. MONGEN NI MANIAWANAI.
Lo! Sitaweza kuwahi muda wa ukomo wa kurudi.

Vidokezo vya sarufi

IIE, SOREHODODEMO

(Hapana, siyo sana.)

IIE ni jibu la kukanusha. SOREHODODEMO inamaanisha "siyo sana." IIE, SOREHODODEMO ni usemi unaotumiwa ukiwa unataka kuonyesha unyenyekevu au kutokuwa na majivuno.

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la NAI
Vitenzi vinavyomalizikia na NAI, vinaitwa "vitenzi vya umbo la NAI."

Tanakali Sauti

Kushangilia
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Nilifikiria Wajapani hawawezi kufurahi hadharani. Lakini sasa ninajua wanapokuwa kwenye mabanda ya Karaoke wanaweza kubadilika. Leo nilihisi tumekuwa marafiki wa karibu.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.