NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 15

Somo la 15

Wamelala.

Anna anaelekea katika duka la kuuza vitabu pamoja na Sakura na Rodrigo. Treni inayowabeba itawasili katika kituo cha Shinjuku muda mfupi kutokea sasa.

Somo la 15 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

NETE IMASU

Mazungumzo

さくら 次は新宿駅です。さあ、降りましょう。 Kituo kinachofuata ni Shinjuku. Sasa, tushuke.
Sakura TSUGI WA SHINJUKU EKI DESU. SÂ, ORIMASHÔ.
Kituo kinachofuata ni Shinjuku. Sasa, tushuke.
ロドリゴ あれ。あの人たち、寝ています。 Hee! Wale watu wamelala. 
Rodrigo ARE. ANO HITO TACHI, NETE IMASU.
Hee! Wale watu wamelala. 
アンナ 大丈夫かな。 Sijui wote watakuwa sawasawa?
Anna DAIJÔBU KANA.
Sijui wote watakuwa sawasawa?
さくら 大丈夫、大丈夫。ほら、起きた。 Hawana shida. Tazama! Wameamka.
Sakura DAIJÔBU, DAIJÔBU. HORA, OKITA.
Hawana shida. Tazama! Wameamka.

Vidokezo vya sarufi

  MASHÔ

Ikiwa utabadilisha MASU kuwa MASHÔ, utatoa pendekezo. Unaweza kusema hivi ikiwa una uhakika ya kwamba wenzako hawatapinga pendekezo lako.
k.m.)
KOKO DE ORIMASU. (Tutashuka hapa.)
>> KOKO DE ORIMASHÔ. (Tushuke hapa.)

Ikiwa unataka kutoa pendekezo huku ukiwauliza wengine kama watakubali au la, unaweza kusema  __MASEN  KA, badala ya   __MASHÔ.  Angalia somo la 13.

Kienzi cha umbo la TE + IMASU

Ikiwa utaongeza IMASU baada ya kitenzi cha umbo la TE, unasema tendo fulani linaendelea.
k.m.)
WATASHI WA GOHAN O TABEMASU. (Nakula chakula.)
>> WATASHI WA GOHAN O TABETE IMASU. (Ninakula chakula.)

Mwalimu Tufundishe

Vivumishi vya umbo la kukanusha
Katika somo la 13, tulijifunza ya kwamba kuna aina mbili za vivumishi vya Kijapani, vivumishi vya I na vivumishi vya NA.

Tanakali Sauti

Kulala
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Treni nchini Japani huwa zinakwenda kwa muda na ni usafiri unaoweza kuutumia kwa urahisi. Lakini hatutakiwi kuzungumza na simu za mkononi kwenye treni. Inabidi niwe muangalifu.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.