NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 12

Somo la 12

Ulikuja lini nchini Japani?

kuna karamu inayofanyika katika bweni la wanafunzi wa kigeni ambako Anna anaishi. Anamtambulisha Rodrigo, mwanafunzi mwenzake kutoka Mexico, kwa SAKURA.

Somo la 12 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

ITSU NIHON NI KIMASHITA KA

Mazungumzo

さくら ロドリゴさんはいつ日本に来ましたか。 Rodrigo, ulikuja lini nchini Japani?
Sakura RODORIGO-SAN WA ITSU NIHON NI KIMASHITA KA.
Rodrigo, ulikuja lini nchini Japani?
ロドリゴ 3月に来ました。 Nilikuja mwezi wa tatu.
Rodrigo SANGATSU NI KIMASHITA.
Nilikuja mwezi wa tatu.
さくら もう日本の生活に慣れた? Umeshazoea maisha ya Japani?
Sakura MÔ NIHON NO SEIKATSU NI NARETA?
Umeshazoea maisha ya Japani?
ロドリゴ ええ、まあ。 Ndiyo, kwa kiasi fulani.
Rodrigo Ê, MÂ.
Ndiyo, kwa kiasi fulani.

Vidokezo vya sarufi

Miezi

Ili kujifunza majina ya miezi, tafadhali angalia "Nyenzo za kujifunzia."

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la TA
Vitenzi vya umbo la TA ni aina ya vitenzi vilivyonyambuliwa ambavyo vinaishia na TA au DA. Ni vya wakati uliopita au wakati timilifu. Hebu nikuelezee vile unavyoweza kubadilisha vitenzi vya umbo la MASU hadi umbo la TA .

Tanakali Sauti

Kelele za kundi la watu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kila mmoja amependa mchuzi wa kari niliopika wa asili ya Thailand. Nimesikia Japani kuna aina ya kari za mtindo wa kwao ambazo ni maarufu sana kwa watoto.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.