NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Kujifunza Kijapani kwa mtandao > Somo la 10 Asante sana kwa wema wenu.
Kujifunza Kijapani kwa mtandao Somo la 10 Asante sana kwa wema wenu.
Kuon san atakwenda kufanya mauzo ya bidhaa mpya kwa kampuni mteja wiki ijayo. Kabla ya hapo, ameazimia kupiga simu kuhakikisha siku na saa za miadi.
Misemo muhimu: ITSUMO O-SEWA NI NATTE ORIMASU
| 取引先 | いつもお世話になっております。 | Asante sana kwa wema wenu. |
|---|---|---|
| kampuni mteja | ITSUMO O-SEWA NI NATTE ORIMASU. | |
| クオン | こちらこそ、お世話になっております。 メールの件ですが、火曜日でよろしいでしょうか? | Hata na sisi, asante sana. Kuhusu jambo lililotajwa katika baruapepe, Jumanne inafaa? |
| KUON | KOCHIRA KOSO O-SEWA NI NATTE ORIMASU. MÊRU NO KEN DESU GA, KAYÔBI DE YOROSHII DESHÔ KA? | |
| 取引先 | はい。お待ちしております。 | Ndiyo. Nitasubiri. |
| kampuni mteja | HAI. O-MACHI SHITE ORIMASU. | |
| クオン | では、火曜日にうかがいます。 失礼します。 | Basi, nitakuja Jumanne. Kwa heri. |
| KUON | DEWA, KAYÔBI NI UKAGAIMASU. SHITSUREI SHIMASU. |
Vidokezo kuhusu Japani (じょうたつのコツ)
Ukijenga uhusiano mzuri na watu wa kampuni yako, yaani wakubwa zako na wenzako, basi utaweza kufanya kazi vizuri zaidi.Wakati wa asubuhi, utatamka kwa uchangamfu OHAYÔ GOZAIMASU, 'Sabalkheri' au 'Habari ya asubuhi?'. Wenzako na wadogo zako unaweza kuwaamkia kwa ufupi na urafiki OHAYÔ ambayo ni kifupisho cha OHAYÔ GOZAIMASU. Wakati wa kumpa mtu pole kwa kazi, utasema O-TSUKARE SAMA DESHITA!, 'Pole kwa kazi.' Wakati wa kuondoka kazini, utasema O-SAKI NI SHITSUREI SHIMASU, 'Natangulia, kwa heri.' GO-KURÔ
SAMA DESU! maana yake vile vile 'Pole kwa kazi,' lakini ni usemi wa kuwapa wadogo zako pole kwa kazi, kwa hivyo haifai kusema kwa wakubwa zako!
Kutafuta kwa kutumia mada
- Ushauri, maoni na maombi
- Kuomba muongozo na maelezo
- Misemo inayotumika sana
- Kuelezea hali halisi
- Kutoa maoni
- Kusalimiana
- Misemo ya adabu
- Kujibu
- Kujitambulisha
- Kufanya manunuzi
RSS
Kuangalia zaidi
Bookmark
![[Bure] Kutafuta na kuhifadhi masomo (Sauti /Maandishi)](../../images/btn_dl.png)