NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Tujue kuhusu “Podcasting”
Tujue kuhusu “Podcasting”
“Podcasting” ni kitu gani?
Podcasting ni mfumo wa ku-download yaliyomo kutoka vyanzo mbali mbali ikiwa ni pamoja na redio za interneti katika computer binafsi na kusikiliza kupitia kompyuta binafsi, au kifaa cha kusikilizia ambacho unaweza kwenda nacho popote. Inakuwezesha kusikiliza yaliyomo ambayo ume-download kwa njia ambayo unasikiliza kifaa cha mkononi cha kusikilizia. Ili uweze kupokea vipindi unavyovipenda vya podcasting, unahitaji kujisajili kwa vituo vya redio za internet, au vyanzo vingine kupitia sehemu ya programu maalum ya kompyuta. Kisha utapata tukio la karibuni kabisa la kila kipindi kilichohifadhiwa katika kompyuta yako ya binafsi-PC, kadiri inavyopatikana kwa sababu programu hiyo moja kwa moja inafanya download ya onyesho hilo. Unaweza kusikiliza yaliyomo unayopenda, kwa wakati unaotaka na mahali unapopataka, kama vile katika treni unapoenda au kutoka kazini.
Namna ya kusikiliza “Podcasting”
Ili kufurahia matangazo ya podcast, unahitaji kuwa umeunganishwa na mawasiliano ya internet na uwe na programu maalum kwaajili ya kupokea mawasiliano ya dijitali (e.g. iTunes). Fanya download ya programu maalum inayohusiana na vipindi hivyo, kisha programu hiyo itafanya dowonload moja kwa moja ya kila tukio jipya. Unaweza kusikiliza tukio hilo baadaye wakati unapotaka ikiwa utahamishia katika kifaa chako cha mkononi cha kusikilizia cha mawasiliano ya dijitali.
Ikiwa una iTunes
Usajili unakamilika unapoburuta na kudondosha kitufe kwenye skrini ya podcast ya iTunes. Unaweza kufurahia mambo yaliyomo unayoyapenda, wakati unaotaka ikiwa utahamishia katika kifaa chako cha kusikilizia cha mkononi cha mawasiliano ya dijitali. Matukio ya zamani yaliyohifadhiwa katika podcast nafasi zake huchukuliwa moja kwa moja na matukio ya karibuni zaidi mara tu yanapoingia.
RSS
Kuangalia zaidi
Bookmark
![[Bure] Kutafuta na kuhifadhi masomo (Sauti /Maandishi)](images/btn_dl.png)